MNYAMA AKATAA UNYONGE DHIDI YA MTANI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Simba SC imevunja uteja dhidi ya watani wao Yanga SC baada ya kutoka sare ya 0-0 katika dabi kariakoo iliyopigwa kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar.

Mnyama aliingia kwenye mchezo huo akiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo sita iliyopita dhidi ya Yanga, lakini safari hii alionyesha sura mpya kwa kupambana kwa nguvu zote na kukataa uteja wa kufungwa.

Simba waliutawala mchezo kuanzia kipindi cha kwanza, wakitengeneza nafasi nyingi za mabao kuliko matarajio ya wengi, Takwimu zinaonyesha Simba walipiga mashuti 12, kati ya hayo sita yakilenga lango, wakati Yanga wakipiga mashuti saba , mawili yakilenga lango.

Mchezo huo ulikuwa wa kuvutia kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, kila upande ukionyesha nia ya kutafuta ushindi ingawa hakuna aliyefanikiwa kuvunja ukuta wa mwenzake.

Kwa ujumla, dabi hiyo imeashiria kurejea kwa ushindani mkali uliokuwa umepotea kwa miaka kadhaa, huku ubora wa vikosi vya timu zote mbili ukichochea mvuto mpya wa pambano hilo kubwa la soka Tanzania.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments