Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kesho kuivaa Manchester City katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Mbappe tayari amerejea kufanya mazoezi baada ya kuwa nje kutokana na majeraha, lakini bado hajafikia utimamu wa asilimia mia moja unaohitajika kuweza kucheza dhidi ya City.
Kutokuwepo kwa nyota huyo kunatajwa kuwa pigo kwa Real Madrid, hasa ikizingatiwa ubora wake katika safu ya ushambuliaji na mchango wake mkubwa katika michezo ya hivi karibuni ya klabu hiyo.
Wakati Madrid wakimkosa Mbappe, upande wa Manchester City wamepata nafuu baada ya mshambuliaji wao tegemeo Erling Haaland kurejea kwenye kikosi na anatarajiwa kuwepo kesho kuiongoza safu ya ushambuliaji ya City katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment