MBAPPE AREJEA MAZOEZINI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Kylian Mbappe, amerejea mazoezini baada ya kukosa michezo kadhaa kutokana na majeraha.

Mbappe alionekana akifanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake katika maandalizi ya michezo ijayo ya timu hiyo, hatua inayoongeza matumaini kwa mashabiki wa Real Madrid kumuona nyota huyo akirejea uwanjani hivi karibuni.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa nje ya uwanja kwa muda akiponya jeraha lililomfanya kukosa baadhi ya michezo muhimu ya timu yake.

 Hata hivyo, kurejea kwake mazoezini kunaashiria kuwa anaendelea vizuri na huenda akawa tayari kurejea katika kikosi cha Real Madrid katika mechi zijazo iwapo ataendelea kuwa fiti huku akitarajiwa kupata walau dakika kadhaa za kucheza katika michezo ya hivi karibuni ikiwemo mchezo wa UCL dhidi ya Man city.

0767815463,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments