MBAPPE ABIKIZA MABAO MAWILI KUWA MFUNGAJI WA MUDA WOTE UFARANSA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe, ameendelea kuthibitisha ubora wake kimataifa baada ya kusogea karibu kuivunja rekodi ya mabao ya muda wote ya timu hiyo inayoshikiliwa na Olivier Giroud.

Mbappe sasa amefikisha mabao 56, akibaki bao moja tu kufikia rekodi ya Giroud mwenye mabao 57, huku Thierry Henry akishika nafasi ya tatu kwa mabao 51.

Katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa usiku wa Machi 26, 2026, Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi timu ya taifa ya Brazil ambapo Mbappe alifungua ukurasa wa mabao mapema, akionyesha makali yake langoni kabla ya Hugo Ekitike kuongeza bao la pili lililohakikisha ushindi kwa Ufaransa.

Kwa sasa Mbappe amebakiza bao mbili pekee kuwa mfungaji bora wa muda wote huku akiwa kijana zaidi, kitu ambacho kinaenda kutengeneza historia nyingine ambayo itakuwa ngumu zaidi kuvunjwa kwa kuzingatia bado kijana na anamichezo mingi zaidi ya kucheza.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments