MAJOGOO WAMKOSA ALISSON BECKER

 

Timothy Lugembe

Mwanakwetusports.

Klabu ya Liverpool FC imethibitisha kuwa kipa wake namba moja, Alisson Becker, hajajumuishwa katika kikosi kilichosafiri kuelekea Uturuki kwa ajili ya mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Galatasaray.

Taarifa zinaeleza kuwa kipa huyo wa kimataifa wa Brazil ameondolewa katika kikosi hicho kutokana na kutokuwa katika utimamu mzuri wa mwili (fitness), hali iliyomfanya kubaki England huku wachezaji wenzake wakisafiri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo muhimu wa michuano ya Ulaya.

Mbali na Alisson, Liverpool pia itawakosa wachezaji wengine katika mchezo huo ambao ni Conor Bradley, Federico Chiesa, pamoja na Alexander Isak, ambao nao hawatajumuika na kikosi kitakachomenyana na Galatasaray.

Kutokuwepo kwa nyota hao kunatajwa kuwa pigo kwa Liverpool kuelekea pambano hilo, huku benchi la ufundi likitarajiwa kufanya marekebisho ya kikosi ili kuhakikisha timu inabaki na ushindani katika uwanja wa ugenini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments