Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kijana mwenye umri wa miaka 16 wa Arsenal, Max Dowman, ameandika historia ya kipekee katika Premier League baada ya kuwa mchezaji kijana zaidi kufunga bao katika ligi hiyo.
Dowman alifanya hivyo katika dakika za mwisho kabisa za nyongeza 90+7 kwenye mchezo dhidi ya Everton, akifunga bao muhimu lililo wahakikishia The gurners ushindi na alama tatu muhimu.
Bao hilo la dakika za jioni lilikuwa kama mpira wa mwisho wa mchezo, likiwasha shangwe kubwa kwa mashabiki wa Arsenal na kumfanya kijana huyo kuingia moja kwa moja kwenye vitabu vya historia ya ligi hiyo, kwenye nyakati za asali na maziwa wakati wakibakiza hatua chache kutwaa taji la ligi hiyo.
Mbali na rekodi hiyo ya kipekee, ushindi huo pia unaendelea kuipa Arsenal matumaini makubwa ya kuusogelea ubingwa wa Premier League baada ya kusubiri kwa muda mrefu, huku nyota huyo chipukizi akionyesha kuwa anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa baadaye ndani ya kikosi hicho.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment