Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka nchini Guinea limeibua mjadala mzito kufuatia taarifa za Shirikisho la mpira wa miguu barani African (CAF) kuhusiana na maamuzi ya ubingwa wa mataifa ya Afrika, likitaka haki itendeke kwa kuangalia matukio ya kihistoria mara baada ya shirikisho Hilo kuwapokonya ubingwa Senegal na kuwapatia Morocco.
Kupitia kauli yao, Guinea wamedai kuwa ikiwa kweli CAF inaweza kupitia upya na kubadili maamuzi ya mashindano ya hivi karibuni kama AFCON 2025, basi isiwe tabu kurejea pia matokeo ya AFCON 1976 ambapo wanadai kulikuwa na mazingira yenye utata.
Kwa mujibu wa hoja hiyo, Guinea wanarejea mchezo muhimu dhidi ya Morocco uliochezwa nchini Ethiopia, wakieleza kuwa kulikuwa na matukio yaliyoacha maswali mengi, Inadaiwa Morocco waliwahi kutoka nje ya uwanja kwa muda wakipinga bao la awali lililofungwa na mshambuliaji Cherif Souleymane, kabla ya kurejea na baadaye kusawazisha na kufanya matokeo yawe 1-1.
Matokeo hayo yaliifanya Morocco kutwaa ubingwa huo kutokana na mfumo wa mashindano uliotumika wakati huo, jambo ambalo Guinea wanaamini halikutenda haki kwao, kwani walihitaji ushindi ili kutwaa taji hilo.
Guinea sasa wanaitaka CAF kufungua upya jalada la tukio hilo, wakisisitiza kuwa haki haipaswi kuwa na mipaka ya muda, hasa inapohusisha heshima na historia ya soka la bara la Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment