Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kenya ipo kwenye wakati mgumu wa kuendelea kushikilia haki ya kuandaa mashindano ya AFCON 2027 baada ya ripoti za hivi karibuni kuonyesha kuwepo kwa changamoto kadhaa, hasa kwenye eneo la miundombinu ya viwanja na ufadhili wa maandalizi.
Taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zimeibua wasiwasi mkubwa kuhusu kiwango cha utayari wa nchi hiyo, huku ikielezwa kuwa baadhi ya viwanja vilivyopendekezwa bado havijafikia viwango vinavyotakiwa kwa mashindano ya kimataifa.
Miongoni mwa viwanja vinavyoangaziwa ni pamoja na Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani, Nyayo pamoja na Talanta Sports Complex, ambavyo vinadaiwa kuhitaji maboresho makubwa ili kukidhi vigezo vya CAF kabla ya muda wa mwisho kufika.
Kutokana na hali hiyo, Kenya imepewa masharti kadhaa muhimu ya kutekeleza ndani ya muda maalum kabla ya tathmini nyingine kufanyika, hatua itakayotoa uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya uenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Iwapo maboresho hayo hayatatekelezwa kwa wakati, kuna uwezekano mkubwa kwa Kenya kupokonywa haki ya kuandaa AFCON 2027, jambo ambalo litakuwa pigo kwa ndoto za taifa hilo kujitangaza kimataifa kupitia soka
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment