KADI ZA NJANO ZAMUWEKA GUARDIOLA NJE

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha wa Manchester City , Pep Guardiola, amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa michezo miwili baada ya kufikisha jumla ya kadi sita za njano.

Guardiola alipata kadi yake ya sita ya njano katika mchezo wa FA Cup dhidi ya Newcastle United ambapo Manchester City iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kutokana na adhabu hiyo, Guardiola hatakuwepo kwenye eneo la benchi la ufundi katika michezo ijayo ya City dhidi ya Chelsea na West Ham United.

Kocha huyo atarejea kuingoza City kwenye benchi la ufundi kwenye mchezo wa fainali ya EFL dhidi ya Arsenal.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments