ISSA SY AZIMA VURUGU ZA WAARABU NA KADI NYEKUNDU MKONONI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza uliochezwa Machi 16, 2026 kati ya Esperance de Tunis na Al Ahly SC ulimalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa wenyeji Esperance .

Baada ya filimbi ya mwisho, kulionekana dalili za mvutano kutoka kwa wachezaji wa timu zote mbili kama ilivyo ada ya michezo mingi inayohusisha timu za kiarabu iwapo matokeo au maamuzi ya refa hayata wafurahisha mara nyingi huleta vurugu.

 Hata hivyo mwamuzi kutoka Senegal Issa Sy alisimama imara akiwa na kadi nyekundu mkononi, akionyesha wazi kuwa yuko tayari kumtoa nje mchezaji yeyote ambaye angeanzisha vurugu.

Hatua hiyo iliwafanya wachezaji kuwa waangalifu zaidi, hasa wakizingatia kuwa bado kuna mchezo wa marudiano. Kwa hofu ya kuonyeshwa kadi nyekundu na kukosa mchezo unaofuata, wachezaji walituliza jazba zao na hali ikadhibitiwa haraka.

Uamuzi na msimamo wa mwamuzi huyo ulisaidia kumaliza mchezo kwa utulivu, akionyesha uwezo mkubwa wa kudhibiti joto la mchezo mkubwa kama huo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments