Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limeamua kuibakiza Iran nchini Marekani kwa ajili ya kucheza michezo yake katika Kombe la Dunia 2026.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya ombi la Iran la kutaka kuhamishia michezo yake kwenda Mexico kukataliwa, licha ya taifa hilo kueleza wasiwasi wa kiusalama na hali ya kisiasa.
Taarifa zinaeleza kuwa FIFA imezingatia maandalizi yaliyokwisha fanyika, ikiwa ni pamoja na upangaji wa ratiba na mauzo ya tiketi, hali iliyofanya iwe vigumu kufanya mabadiliko ya ghafla bila kuathiri mwenendo wa mashindano.
Baadhi ya michezo ya Iran itapigwa katika miji ya Los Angeles na Seattle, kama ilivyopangwa tangu awali na inabidi iwe kama ilivyo pangwa ilikuondoa usumbufu kwa timu shiriki zilizopo kundi Moja na Iran.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment