IRAN YABADILI MSIMAMO, SASA YAOMBA MICHEZO YAKE IHAMISHIWE MEXICO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya Iran imebadili msimamo wake baada ya awali kueleza kutoshiriki FIFA World Cup 2026, na sasa imewasilisha ombi kwa FIFA kutaka baadhi ya mechi zake zihamishiwe Mexico badala ya kuchezwa Marekani.

Uamuzi huo unatajwa kuchochewa na wasiwasi wa hali ya usalama na mvutano wa kisiasa baina ya nchi hizo mbili, huku Iran ikisisitiza kuwa ipo tayari kushiriki mashindano hayo endapo mazingira yatakuwa rafiki zaidi.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kufanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu Marekani, Mexico na Canada, lakini hadi sasa FIFA haijatoa maamuzi rasmi kuhusu ombi hilo la Iran.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments