IRAN KUTOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Serikali ya Iran imetangaza kuwa haitashiriki mashindano ya FIFA World Cup itakayo fanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu ambazoni Marekani, Mexico na Canada kufuatia hali ya kisiasa na usalama inayoendelea kuikabili nchi hiyo kwa sasa.

Waziri wa Michezo wa Iran, Ahmad Donyamali, amesema mazingira yaliyopo kwa sasa hayaruhusu taifa hilo kushiriki katika mashindano hayo makubwa ya soka duniani.

Akizungumza kupitia taarifa rasmi, Donyamali alieleza kuwa uhusiano wa Iran na United States pamoja na changamoto za kiusalama zimefanya iwe vigumu kwa nchi hiyo kuandaa ushiriki wake katika Kombe la Dunia.

Aidha, aliongeza kuwa taifa hilo limekumbwa na migogoro mikubwa ya kijeshi katika miezi ya hivi karibuni iliyosababisha vifo vya maelfu ya raia, hali inayofanya serikali kuona si wakati sahihi kushiriki mashindano ya kimataifa ya michezo.

Iwapo uamuzi huo utathibitishwa rasmi na FIFA, unaweza kuwa na athari kubwa katika maandalizi na muundo wa mashindano ya Kombe la Dunia, hususan katika upangaji wa timu zitakazoshiriki mashindano hayo

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments