Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, ameipa moyo timu ya Dar City inayoendelea kushiriki michuano ya Basketball Africa League (BAL) 2026 nchini Afrika Kusini.
Dkt.Kikwete alikutana na wachezaji hao akiwa kwenye ziara yake jijini Pretoria, akiwahimiza kuendelea kupambana na kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa wakiongozwa na mchezaji nguli Hasheem Thabiti.
Dar City imeanza vyema michuano hiyo baada ya kushinda michezo miwili ya awali, hali inayowapa matumaini makubwa ya kufuzu hatua ya robo fainali.
Katika mchezo unaofuata, timu hiyo itakutana na Al Ahly Benghazi, ambapo ushindi uta afanya kufuzu hatua ya robo fainali michuano hiyo.
Hamasa kwa Dar city imekuwa kubwa kutokana na kufanya kwao vizuri ambapo kwenye michezo Yao wameshuhudiwa viongozi wakubwa nchini wakisafiri Hadi Afrika kusini kwaajili ya kuwaunga mkono na hii Leo ilikuwa ni zamu ya Rais mstaafu kutia baraka zake
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment