DER KLASSIKER YAGEUKA MAUMIVU KWA DORTMUND , KANE AGEUKA TISHIO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Bayern Munich imeendelea kujiimarisha kileleni mwa Bundesliga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika dabi ya Der Klassiker iliyochezwa Signal Iduna Park hapo Jana.

Ushindi huo umeifanya Bayern kutengeneza pengo la alama 11 juu ya kilele cha msimamo, huku pia ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Dortmund kupoteza wakiwa nyumbani msimu huu wa ligi.

Dortmund walionyesha ushindani mkubwa lakini walishindwa kuwazuia Bayern hadi dakika za mwisho ambapo Bayern walikamilisha kazi na kuondoka na alama zote tatu muhimu.

Mshambuliaji wa Bayern , Harry Kane anazidi kuwa tishio mbele ya mabeki wa timu pinzani baada ya kuchangia kufunga mabao mawili kwenye ushindi huo, mpaka sasa ana mchango wa mabao 35, akifunga mabao 30 na assist 5, huku anaemfuatia kwenye msimamo akiwa na mabao 13 tofauti ya mabao 27.

Wafungaji:

Dortmund – Schlotterbeck 26’, Svensson 83’

Bayern Munich – Kane 54’, Kane (P) 70’, Kimmich

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments