Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
kiungo nyota wa Manchester United, Casemiro, amethibitisha rasmi kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake.
Casemiro amesema bado anafurahia kuitumikia Manchester United, lakini tayari ameshafanya maamuzi magumu ya kuachana na timu hiyo, Kiungo huyo mkongwe ameweka wazi kuwa upendo mkubwa kutoka kwa mashabiki umemgusa sana, lakini haujabadilisha uamuzi wake wa kuondoka.
Katika kipindi cha hivi karibuni, Casemiro amekuwa katika kiwango bora akichangia matokeo chanya ya timu hiyo, hali iliyowafanya mashabiki wengi kuomba aongezewe mkataba wa mwaka mmoja zaidi ili aendelee kubaki klabuni hapo, hata hivyo, juhudi hizo hazijazaa matunda baada ya nyota huyo kusisitiza kuwa tayari ameshaamua hatima yake.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekiri kuwa michezo yake ya mwisho akiwa na jezi ya Manchester United itakuwa na hisia kali, akieleza kuwa yuko tayari kukabiliana na wakati huo mgumu.
Kuondoka kwake kunatarajiwa kuacha pengo kubwa ndani ya kikosi hicho, hasa kutokana na uzoefu na mchango wake uwanjani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment