Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Arsenal imejikuta ikipoteza kikombe cha kwanza msimu huu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Manchester City kwenye fainali ya Carabao Cup iliyofanyika uwanja wa Wembley na City kutwaa taji hilo.
Matokeo hayo yana maanisha kuwa Arsenal sasa wamebakiwa na mashindano matatu pekee ya kuwania msimu huu, ambayo ni Premier League, UEFA Champions League pamoja na FA Cup.
Hata hivyo, uzito mkubwa wa matumaini yao unaelekezwa zaidi kwenye Ligi Kuu England (EPL), ambapo wana nafasi kubwa ya kupambana kutwaa ubingwa, huku mashabiki wakiamini hilo ndilo taji linaloweza kufuta maumivu ya miaka mingi bila ubingwa.
Kwa sasa, safari ya Arsenal inaendelea, lakini presha imeongezeka huku imani juu ya kutwaa taji Moja wapo msimu huu ikiwa juu tofauti na misimu ya nyuma.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment