ARSENAL VINARA KUTWAA UCL KWA MUJIBU WA TAKWIMU

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya michezo ya hatua ya awali na 16 Bora , timu nane zimefuzu hatua ya robo fainali na na kulingana na viwango vyao utabiri wa timu itakayo Fanya vizuri umefanyika kwa mtiririko wake kwa kuzingatia takwimu.

Kwa mujibu wa mwenendo wa sasa wa mashindano haya, Arsenal wameibuka kama timu iliyo imara zaidi, wakionyesha kiwango cha juu katika vipengele vyote muhimu, ushambuliaji, ulinzi na udhibiti wa mchezo.

 Ndani ya michezo yao ya UCL pekee, Arsenal wamefanikiwa kushinda yote, wakifunga mabao 26 na kuruhusu mabao 5 tu, takwimu inayowaweka juu kwa uimara wa safu ya ulinzi, wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa ikichagizwa na kuzifunga timu mbili zilipo robo fainali sasa kwa idadi nzuri ya mabao walishinda 3-1 dhidi ya Beyern Munich, na 4-0 dhidi ya Atletico Madrid , taswira hii Inaonyesha wanawamudu vigogo.

Kwa upande mwingine, Barcelona wanaongoza kwa upande wa ushambuliaji wakiwa na mabao 30, lakini udhaifu wao uko kwenye safu ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao 17 ,hali inayowafanya kuwa timu ya hatari lakini inayofikika.

Bayern Munich wao wameendelea kuwa na uwiano mzuri kati ya kushambulia na kulinda, wakibaki kuwa moja ya timu zenye uwezo mkubwa wa kufika hatua ya mwisho kutokana na uzoefu wao na uwezo wa kufunga mabao kwa ufanisi mkubwa.

Hata hivyo, licha ya takwimu hizi zote, macho mengi bado yanaelekezwa kwa Real Madrid mabingwa wa kihistoria, Klabu hiyo ya Hispania imeendelea kuthibitisha kuwa si lazima iwe bora kwa takwimu ili kushinda taji, bali uzoefu wao mkubwa katika hatua za mtoano huwafanya kuwa timu ya kuogopwa zaidi Uwezo wao wa kushinda michezo migumu kwa ufanisi mkubwa unawapa nafasi ya kipekee hata wanapokuwa hawapo kwenye kiwango bora cha takwimu.

Timu nyingine ni Paris Saint-Germain na Liverpool zinaendelea kuonyesha ushindani, lakini bado zinakabiliwa na changamoto za kutokuwa na uthabiti, huku Atletico Madrid wakibaki kuwa timu ya kiufundi zaidi Katika michezo yake

Kwa upande wa Sporting CP, wao wamefika hatua hii kama underdog, lakini tofauti ya ubora dhidi ya vigogo wa Ulaya bado inaonekana wazi na kibarua kilichopo mbele Yao ni Arsenal ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji.

Hizi ni takwimu lakini mpira wa miguu ni mchezo wa dakika 90, lolote linaweza kutokea kinyume na matarajio hivyo kuelekea robo fainali matokeo yatajieleza yenyewe, huenda takwimu zikaongea au zikagoma.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments