ANCELOTTI AFAFANUA SABABU YA KUMWACHA NJE NEYMAR BRAZIL

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, ameeleza sababu ya kutomjumuisha nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr kwenye kikosi cha hivi karibuni.

Ancelotti amesema kuwa Neymar bado hajafikia utimamu wa mwili kwa asilimia 100, jambo lililopelekea kuachwa nje ya kikosi hicho licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa timu hiyo.

Hata hivyo, kocha huyo ameweka wazi kuwa bado ana nafasi ya kuitwa katika Kombe la Dunia 2026 endapo ataendelea kuimarika kimwili.

Brazil imetangaza kikosi hicho kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kalenda ya FIFA, ambapo wanatarajia kuvaana na Ufaransa jijini Boston, Marekani Machi 26, kabla ya kukipiga dhidi ya Croatia siku chache baadaye mjini Orlando.

Kutokuwepo kwa Neymar ni pigo kwa mashabiki wa Brazil, lakini benchi la ufundi linaamini kurejea kwake akiwa fiti kutakuwa na mchango mkubwa zaidi kwa timu hiyo kuelekea michuano mikubwa ijayo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments