Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Droo ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepangwa rasmi, ikitoa michezo mikali kwa vigogo wa soka barani Ulaya.
Macho na masikio ya mashabiki wengi yataelekezwa kwenye pambano la kusisimua kati ya Real Madrid na Manchester City, timu ambazo zinakutana tena katika hatua za mtoano. Miamba hiyo imekuwa na historia ya kukutana mara kwa mara, hivyo pambano hili linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Wakati huo huo, Paris Saint-Germain itakuwa na kazi nzito dhidi ya Chelsea, huku PSG ikiingia kwenye mchezo huo ikiwa bado inajiuliza baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu matokeo yanayoongeza presha kwa miamba hiyo ya Ufaransa na uzito wa mchezo kwa ujumla.
Michezi mingine ni Galatasaray dhidi ya Liverpool, Newcastle United dhidi ya Barcelona, huku Atletico Madrid kukipiga na Tottenham Hotspur.
Nyingine ni Atalanta dhidi ya Bayern Munich, Bodø/Glimt dhidi ya Sporting CP, na Bayer Leverkusen wakikabiliana na Arsenal.
Kwa ujumla, droo hii imeleta vita vya mapema kwa vigogo, huku mashabiki wakisubiri kuona nani ataendelea kusonga mbele kuelekea robo fainali.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment