Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya imekamilika huku vigogo wa soka barani humo wakijiandaa kupambana kusaka tiketi ya robo fainali, Jumla ya timu 16 zimefuzu, na Ligi Kuu England (EPL) imeonyesha ubabe baada ya kutoa timu sita kwenye hatua hii.
Waliopenya ni Arsenal, Liverpool, Tottenham Hotspur, Chelsea, Manchester City na Newcastle United , zote zikitokea EPL na kuifanya ligi hiyo kuwa na uwakilishi mkubwa zaidi katika hatua hii hatua hii.
Kutoka Hispania, miamba Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid wameendelea kuthibitisha ubora wao kwa kusonga mbele
Ujerumani imewakilishwa na Bayern Munich pamoja na Bayer Leverkusen, huku Ufaransa ikipeperusha bendera kupitia Paris Saint-Germain.
Kutoka Italia ni Atalanta, wakati Ureno wakiwakilishwa na Sporting CP. Orodha hiyo inakamilishwa na mabingwa wa Uturuki Galatasaray pamoja na Surprise package wa mashindano, Bodø/Glimt kutoka Norway.
Kwa ushindani ulivyo mkali na vigogo wengi kuendelea, hatua ya 16 bora inatarajiwa kutoa mapambano makali yatakayoamua nani atatinga robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment