Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports,
Kwa mara ya kwanza klabu ya Simba Sc toka ianze kushiriki hatua ya makundi klabu bingwa na Shirikisho kwa miaka ya hivi karibuni imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Esperance de Tunis katika dimba la Benjamin Mkapa.
Mchezo huo ulikua ni mzunguko wa nne ikiwa imesalia michezo miwili huku Simba wakivuna alama Moja pekee jambo ambalo linamfanya akose nafasi ya kufuzu.
kulikuwa na matumaini huenda akivuna alama sita kwenye michezo miwili iliyosalia kungetengeneza nafasi lakini tayali walisha haribu kwenye (Head to Head) kitu ambacho Bado kitawabeba wapinzani wake.
HIVI NDIVYO VILIWAKWAMISHA SIMBA.
Kabla ya msimu huu klabu ilikuwa inajengwa baada ya kuyumba kwa kipindi kifupi na kupoteza ubingwa wa LIGI kuu kwa miaka mitatu, timu ilijengwa chini ya kocha Fadlu ambae alitengeneza kikosi kilicho fika hatua ya Fainali kombe la shirikisho na kupoteza dhidi ya Berkane.
Msimu huu ulipoanza Fadlu aliendelea na kuimarisha timu huku akisajili wachezaji watakao endana na falsafa yake , isivyo bahati alipata ofa kujiunga na Raja Casablanca hivyo klabu ikamuajiri Dimitar Pantev ambaye nae upepo haukumuendea vizuri baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya klabu bingwa.
Klabu iliamua kumuajiri kocha Steve Barker ambaye ndio ane kinoa kikosi mpaka sasa , kiufundi Kila kocha anatamani wachezaji wa aina fulani wa kuendana na falsafa zake hivyo akija kwenye timu atahitaji wachezaji wake kitu kinacho haribu mtindo wa uchezaji wa timu kwa sababu Kila siku wachezaji wanakuja wapya , mwalimu mpya hivyo uimara wa timu unapotea ndio walicho kifanya Simba hadi kukutwa na janga hili.
PRESHA KUTOKA KWA YANGA
Klabu ya Yanga imekuwa imara kwa msimu wa nne mfululizo kitu ambacho kinawapa maswali Simba , Hali ambayo inamfanya mnyama atumie Kila mbinu kumthibiti Yanga , presha hiyo ya Yanga kufanya vizuri imewafanya Simba kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi mara kwa mara nakujikuta Wana feli katika Mipango Yao huku mahasimu wao wakizidi kupeta.
Licha ya klabu kupitia mvurugiko wa benchi la ufundi lakini ukubwa wao uliwabeba walipokuwa uwanjani walicheza vizuri huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini walishindwa kufanya hivyo, kinyume chake wapinzani wao Kila nafasi walitumia kama dhahabu na kuiadhibu klabu hiyo.
Kwenye Kila mchezo Simba kama angetumia nagalau nusu ya nafasi alizozipata Leo hii tusingezumzia kuhusu kutoka kwake kwenye mashindano mapema bali huenda ingekuwa ni timu ambayo imebakiza alama Moja kufuzu.
Simba sio timu mabovu ila inahitaji watu wa mpira wanaojua mchakato wa kuitoa klabu chini na kuirejesha kwenye ushindani, kwa sasa klabu ikae chini itafakari wapi wamekwama wakubaliane na hali na waanzee upya .
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.jpeg)

.jpeg)
Post a Comment