Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester United imeendelea kung’ara kwenye Ligi Kuu England (EPL) mwaka 2026 baada ya kubaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wa ligi tangu kuanza kwa mwaka huu na hiyo ni baada ya hapo Jana kuiadhibu Everton bao 1-0.
Ndani ya michezo nane iliyocheza mpaka sasa mwaka 2026, United imefanikiwa kushinda michezo mitano na kutoka sare tatu, matokeo yaliyowafanya kukwea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi wakiwa nafasi ya nne na alama 48.
Katika kipindi hiki, Mashetani Wekundu wameonyesha uimara mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji kwa kufunga mabao 15, huku wakiruhusu mabao nane pekee takwimu zinazoonesha uwiano mzuri wa timu hiyo katika pande zote mbili.
Matokeo hayo mazuri yameipa United nafasi ya kupanda hadi ndani ya nne bora kwenye msimamo wa ligi, hatua inayofufua matumaini ya kurejea kwenye ushindani mkubwa wa juu msimu huu huku wakitazamiwa kuwa tishio zaidi kwa misimu ijayo.
Kupanda kwa kiwango cha timu hiyo kunahusishwa kwa kiasi kikubwa na ujio wa kocha Michael Carrick, ambaye ameonekana kuibadilisha sura ya kikosi kwa muda mfupi tangu atue kwenye benchi la ufundi, ambapo kiuchezaji mpaka nidhamu ndani ya timu vimekuwa vya hali ya juu, hakuna migogoro kilichopo ni umoja na mshikamano.
Mashabiki wa United sasa wanaanza kurejesha imani yao, wakitarajia mwendelezo wa matokeo chanya kadri mbio za Ligi Kuu England zinavyozidi kupamba moto.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.jpg)
.jpg)
Post a Comment