TUZO ZA MWEZI JANUARI ZAANGUKIA YANGA NA DODOMA JINI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC, William Edgar, ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Januari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 baada ya kuonyesha kiwango kizuri kilichosaidia timu yake kupata matokeo chanya kwenye michezo iliyochezwa mwezi huo.

Edgar alifanikiwa kufunga mabao matatu kwenye michezo minne iliyochezwa mwezi Januari ambapo alichangia alama 7 kwa klabu yake na kuwashinda Fabrice Ngoy wa Namungo pamoja na Laurindo Aurelio ‘Depu’ wa Young Africans, walioingia naye fainali katika mchakato wa tuzo hizo.

Kocha wa Yanga Africans SC, Pedro Goncalves, ametangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Januari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, kufuatia uongozi wake mahiri ulioiwezesha timu hiyo kushinda michezo miwili kwa idadi kubwaa ya mabao(9)

Chini ya Goncalves, Yanga Africans waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na ushindi mkubwa wa 6-0 dhidi ya Mashujaa FC, Kocha huyo aliwashinda Juma Mgunda wa Namungo na Yusuph Chipo wa Mtibwa Sugar, walioingia naye fainali katika tuzo hizo za mwezi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com,


0/Post a Comment/Comments