Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Tottenham Hotspur imemteua rasmi kocha raia wa Croatia, Igor Tudor, kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tudor amekubali ofa ya kuinoa Spurs hadi majira ya joto, huku makubaliano yakielezwa kudumu hadi Juni 2026, lakini akitarajiwa kusalia hadi mwisho wa msimu huu kabla ya uamuzi wa kudumu kufanyika.
Uteuzi huo unatajwa kuwa wa muda, wakati uongozi wa Tottenham ukiendelea kupima chaguo la kocha wa kudumu atakayeanza kazi rasmi msimu ujao.
Wakati huo huo, makocha wawili wakubwa barani Ulaya, Roberto De Zerbi na Mauricio Pochettino, wametajwa kuwa wagombea wakuu wa kibarua cha kudumu kitakachoanza majira ya joto.
Uongozi wa Spurs unatarajiwa kufanya tathmini ya kina kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kuona kama Tudor ataweza kuibadilisha timu hiyo katika kipindi chake cha muda mfupi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment