TER STERGEN AKUMBWA NA MAJERAHA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Golikipa wa klabu ya Girona, Marc Andre Ter Stegen, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya kupata jeraha kubwa la misuli ya paja (hamstring).

Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu, jeraha hilo ni kubwa kiasi cha kuhitaji upasuaji, hatua inayolenga kuhakikisha anarejea akiwa katika hali bora kiafya.

Inakadiriwa kuwa Ter Stegen atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili hadi minne, kutegemeana na taarifa za kitabibu zitavyoekeza.

Kutokuwepo kwa kipa huyo ni pigo kwa Girona ambao walimsani kutoka Barcelona kipindi kifupi nyuma kwaajili ya kuimarisha kikosi hicho, benchi la ufundi sasa litalazimika kufanya marekebisho, huku walinda mlango wengine wakipewa nafasi ya kuonyeshwa ubora wao.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments