Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imelaani vikali vitendo vya vurugu vilivyofanywa na na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu hiyo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu, baada ya mchezo dhidi ya Esperance ya Tunisia uliochezwa February 01, 2026 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Crescentius Magori, klabu hiyo imesema vitendo hivyo ni vya kinyama, havikubaliki kabisa na havina nafasi katika michezo wala jamii yenye ustaarabu.
“Uongozi wa Klabu unatoa pole kwa Mwenyekiti Mangungu kwa kadhia hiyo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, uongozi wa Simba umeeleza kuwa tayari umelishirikisha Jeshi la Polisi ili kuhakikisha wahusika wote waliohusika katika vurugu hizo wanachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.
Bodi ya Wakurugenzi imesisitiza kuwa haitavumilia mtu au kikundi chochote kinachojaribu kuharibu taswira na heshima ya Klabu ya Simba, huku ikiahidi kuendelea kulinda maadili, amani na usalama ndani na nje ya viwanja vya michezo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment