SIMBA WANAIMANI NA ALAMA TATU ZA PETRO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imeweka wazi dhamira yake ya kusaka matokeo chanya ugenini itakapokabiliana na Atlético Petróleos de Luanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mzunguko wa tano.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Neo Maema amesema kikosi hicho kimejifunza mengi katika michezo miwili iliyopita na sasa kimefanya maboresho makubwa.

“Wachezaji tunafahamu si rahisi kucheza na Petro ugenini, ila ndani ya timu yetu kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye mechi mbili zilizopita tumecheza vizuri na naamini tutakuwa na muendelezo huo pamoja na kupata ushindi ugenini,” alisema Maema.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Simba ikilenga kuvunja mwiko wa ushindi kwenye mashindano haya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments