Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo uliowakutanisha Manchester United dhidi ya West Ham ulimalizika kwa sare ya 1-1 mchezo ulipigwa Februari 10, 2026, jijini London.
Mbali na matokeo hayo, macho na masikio ya mashabiki wengi yalikuwa kwa shabiki maarufu wa United, Frank Ilett, ambaye aliweka wazi ahadi yake mwezi Oktoba 2024 kwamba hatanyoa nywele zake hadi klabu hiyo itakaposhinda michezo mitano mfululizo.
Kabla ya mchezo dhidi ya West Ham, United walikuwa tayari wameshinda michezo minne mfululizo na walihitaji ushindi mmoja tu kutimiza sharti la Frank, Hata hivyo, sare hiyo imefanya ahadi yake kuendelea kudumu, hali inayomaanisha atalazimika kusubiri tena hadi United watakapofanikiwa kukamilisha ushindi wa michezo mitano mfululizo.
Kabla ya mchezo wa hapo Jana united ilikuwa imeshinda michezo minne mfululizo, na hapo Jana wagonga nyundo walizuia mtiririko huo wa ushindi.
Hadi sasa, Manchester United imeshindwa kufikia malengo hayo tangu ahadi hiyo iwekwe swali ni je, Frank atakaa na hizo nywele mpaka ahadi yake itimie au ata vunja ahadi?
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com




Post a Comment