RICE AWAITA ARSENAL KUSIMAMA PAMOJA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Declan Rice amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwaunga mkono katika kipindi hiki muhimu cha msimu, akisisitiza kuwa umoja ni muhimu katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.

Rice, akizungumza na chombo kimoja cha habari, amesema Arsenal imefika hapo ilipo sasa kwa nguvu ya pamoja kati ya wachezaji na mashabiki, hivyo si wakati wa kugeukiana bali ni muda wa kusimama bega kwa bega.

Alieleza kuwa timu inahitaji kila shabiki kuwa katika mstari mmoja, akiwasihi kuendelea kupambana kwa ajili ya wachezaji na klabu kwa ujumla huku wakidumisha imani kwa kikosi hicho.

Kuhusu mbio za ubingwa wa Premier League, Rice alisisitiza kuwa hawatapewa taji kwa hisani bali wanapaswa kulipigania na kulistahili uwanjani, huku wakijiandaa kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza.

Aidha, kiungo huyo alifichua kuwa kikosi kilifanya kikao cha pamoja kujitathmini na sasa kiko tayari kurejea kwa nguvu mpya katika mapambano ya msimu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments