Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezaji wa SL Benfica, Gianluca Prestianni, atakosekana katika mchezo ujao dhidi ya Real Madrid baada ya kufungiwa kwa mchezo mmoja na Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, UEFA imempa Prestianni adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja wakati uchunguzi ukiendelea kufuatia tuhuma za vitendo vya kibaguzi vinavyodaiwa kumhusisha na nyota wa Madrid, Vinicius Junior.
UEFA imesema inaendelea kuchunguza kwa kina tuhuma hizo, ikisisitiza kuwa inachukulia kwa uzito mkubwa masuala yote ya ubaguzi katika soka la Ulaya. Endapo tuhuma hizo zitathibitishwa, beki huyo anaweza kukumbana na adhabu nzito zaidi ya hadi kufungiwa michezo 10.
Kukosekana kwa Prestianni kunatajwa kuwa pigo kwa Benfica kuelekea mchezo huo muhimu, huku macho ya wadau wa soka yakielekezwa kwa uamuzi wa mwisho wa UEFA baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment