Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans SC, Pedro Goncalves, ameonyesha imani kubwa kwa kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asfar, akisisitiza kuwa Yanga ina wachezaji wenye uwezo wa kucheza katika mazingira tofauti na kupata matokeo.
Akizungumza kabla ya mchezo huo , Goncalves alisema benchi la ufundi limewasoma vizuri wapinzani wao na limejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto zote zitakazojitokeza uwanjani pia timu imefanya maandalizi ya kutosha kwa kuzingatia mbinu na uwezo wa Asfar.
“Hakuna timu bora ambayo haina madhaifu, sisi tunalenga kuyatumia madhaifu yao kupata matokeo, tuna timu bora yenye uwezo wa kushinda hata katika mazingira magumu,” alisema Goncalves.
Kauli hiyo inaongeza matumaini kwa mashabiki wa Yanga, ambao wanatarajia kuona kikosi chao kikiendeleza mwenendo mzuri katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Mchezo dhidi ya Asfar unatajwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku Yanga ikilenga kuondoka na matokeo chanya yatakayoongeza nafasi yao ya kusonga mbele katika mashindano hayo.
0767915474,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment