PARTEY AANDAMWA NA KESI ZA UBAKAJI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezaji wa Villarreal na timu ya Taifa ya Ghana Thomas Partey anaripotiwa kuchunguzwa nchini Uingereza kufuatia malalamiko mawili mapya yanayohusiana na tuhuma za ubakaji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoelezwa na Carrusel Deportivo, mchakato wa kisheria unatarajiwa kuendelea katika Mahakama ya Westminster Magistrates' tarehe 13 March 2026.

Mbali na hilo, kuna kesi nyingine ambayo imepangwa kusikilizwa mwezi Novemba ambayo inahusha masuala hayo hayo ya ubakaji, kabla ya kesi hiyo kusikilizwa amekumbwa na mashtaka mengine.


Kwa sasa, uchunguzi bado unaendelea na hakuna uamuzi wa mahakama uliotolewa kuhusiana na tuhuma hizo kama ni za kweli au la.

Kwa kesi hii mpya inatia mashaka kuwa mchezaji huyo huenda ametenda makosa hayo , kwa sasa uchunguzi unaendelea na malmlaka husika zitakuja na majibu sahihi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments