NOTTINGHAM FOREST YAFUKUZA MAKOCHA WATATU NDANI YA MSIMU

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Nottingham Forest imeendelea kuwa gumzo Ligi Kuu England baada ya kumfuta kazi kocha Sean Dyche ikiwa ni siku 114 tu tangu apewe mikoba ya kuinoa timu hiyo, Dyche anakuwa kocha wa tatu kufutwa ndani ya msimu huu klabuni hapo, hali inayoonesha msukosuko mkubwa ndani ya benchi la ufundi la klabu hiyo.

Awali, Forest ilianza msimu chini ya Nuno Espirito Santo ambaye aliondolewa Septemba 2025, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Ange Postecoglou aliyedumu hadi Oktoba 2025, Sasa Dyche, aliyeteuliwa kurekebisha jahazi hilo, ameondoka Februari 2026 baada ya matokeo yasiyoridhisha.

Dyche raia wa England, amekumbwa na presha kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya, ikiwemo sare tasa dhidi ya Wolverhampton Wanderers siku ya jumatano Februari 11, Matokeo hayo yaliiacha Forest ikiwa alama tatu tu juu ya mstari wa kushuka daraja, hali iliyoongeza hofu kwa uongozi wa klabu.

Hatua ya kufukuza makocha watatu ndani ya msimu mmoja inaweka shinikizo kubwa kwa uongozi wa Forest, huku mashabiki wakisubiri kuona kama mabadiliko hayo yatarejesha matumaini ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

0767915473

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments