Timothy Lugembe,
Sintofahamu iliibuka kwenye mchezo wa UEFA champions league mzunguko wa kwanza hatua ya mtoano baina ya Real Madrid dhidi ya Benfica ambapo Madrid waliibuka na ushindi wa 1-0 wakiwa ugenini siku ya Februari 17, 2025.
Katika mchezo huo mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior alilamikia suala la ubaguzi wa rangi alilofanyiwa na mchezaji wa Benfica Prestianni alisema kuwa mchezaji huyo aliongea maneno yenye ubaguzi kwa kumuita nyani jambo ambalo pia lilikemewa vikali na Kilyan Mbappe akisisitiza kuwa Prestianni kutokana na Kitendo hicho hafai kucheza BERNABEU
Kwa upande wa Jose Mourinho kocha wa Benfica wakati akiongea na waandishi wa habari alijiuliza kwa Nini Kila mara vini akutane na vitendo hivyo.
"Suala hili linatokea mara nyingi kwenye viwanja likimuhusisha mchezaji yule yule Kuna jambo haliko sawa. Nilimwambia Vinicius ulifunga goli la ajabu (zuri) kwanini ulishangilia vile? Kwani huwezi kushangilia goli kwa furaha tu ya kuwa mchezaji Bora kama kawaida? , kwanini linamtokea yeye Kila mara hali hii ndio jambo pekee ambalo siliewi"
Aliongeza kuwa "Prestianni aliniambia jambo Moja na vini aliniambia jambo jingine hivyo sitaki kuchukua msimamo wa Moja kwa Moja" alisema Mourinho.
Alimaliza kwa kusema Benfica sio klabu ya kibaguzi kwani na wao wanawachezaji weusi.
Vinicius amekumbwa na sakata Hilo mara baada ya kufunga bao na kushangilia mbele ya mashabiki wa Benfica kwa aina ambayo hawakuifurasha.
Mchezaji huyo mara nyingi nidhamu yake ndiyo humuweka kwenye matatizo kama hayo kitu muhimu ni Vini kurekebisha nidhamu yake na kuuchukulia mchezo wa mpira ni mchezo wa fair play.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.jpg)


Post a Comment