Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amethibitisha kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Februari 09, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema mkutano huo utafanyika Februari 13, 2026, huku tayari maafisa wa CAF wakianza kuwasili nchini kuanzia leo kwa ajili ya maandalizi ya kikao hicho muhimu.
Makonda amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini ni fursa kubwa kwa Tanzania katika kukuza soka na kuendeleza sekta ya michezo kwa ujumla, ameeleza kuwa hatua hiyo ni kielelezo cha diplomasia imara iliyojengwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo imeifanya Afrika kuiona Tanzania kama nchi salama na yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo.
Mkutano huo unatarajiwa kuzikutanisha mamlaka za juu za soka barani Afrika, huku Tanzania ikiendelea kujiweka katika nafasi muhimu kwenye ramani ya michezo ya kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment