Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha wa klabu ya Namungo yenye maskani yake mkoani lindi , Juma Mgunda hajafurahishwa na maamuzi ya mwamuzi kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Yanga Sc uliopigwa Februari 22, 2026 kwenye dimba la Majaliwa Stadium.
Katika mchezo huo Namungo walikubali kichapo Cha bao 1-0, bao ambalo lilifungwa kwa mkwaju wa penati .
Kocha Mgunda aliitaja penati hiyo kuwa haikuwa sahihi ila mwamuzi aliamuru iwe, tukio lingine likiwa nilile la timu yake kunyimwa mkwaju wa penati ambao kwa tasmini yake aliamini ilipaswa iwe penati.
Kwa upande wa wadau wa soka, wameungana na kocha Mgunda wakiwashutumu marefa kwa kushindwa kutafsiri matukio kwa usahihi, huku Hali hiyo ikitajwa kama ukandamizaji kwa timu ndogo zinapi cheza na timu kubwa.
Kwa malalamiko haya Bodi ya ligi wana jukumu la kuwaonya waamuzi kutokana na uzembe wanaofanya wakati wa kutafsiri Sheria 17 za soka, ili kupunguza malalamiko ya kimaamuzi kwenye ligi kuu ya NBC.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment