MAUZAUZA YAANZA KUELEKEA DABI YA KARIAKOO, BODI YA LIGI IJITATHIMINI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Hali ya sintofahamu imeanza kuelekea dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC itayopigwa machi 1, 2026, kufuatia uamuzi wa kupelekwa kwa mchezo huo visiwani Zanzibar.

 Maswali yameanza kuibuka miongoni mwa wadau na mashabiki wa soka nchini wengi wanahoji ni kwa nini taarifa za awali kuhusu mchezo huo kupigwa Zanzibar zilitolewa mapema na Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, kabla ya uthibitisho rasmi kutoka Bodi ya Ligi, na baadaye Bodi ya Ligi ilithibitisha Kwa kutoa taarifa rasmi za mchezo huo kupigwa Zanzibar, jambo linalozua hisia mseto kwa baadhi ya mashabiki kuwa huenda kulikuwa na mpango ulioandaliwa mapema.

Katika upande mwingine, Simba nao wamehoji uamuzi wa dabi kupelekwa Zanzibar, Kwa kuhoji huko kunatengeneza hofu huenda hatua hiyo ikaathiri mchezo huo kama ilivyotokea msimu uliopita kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Uamuzi huo umewaumiza mashabiki wengi wa mpira nchini, hasa ikizingatiwa kuwa karibu robo tatu ya wapenzi wa soka Tanzania ni mashabiki wa timu hizo na wanatamani kushuhudia mchezo kwani hufanyika mara chache kwa mwaka hivyo ni kama wamenyimwa haki Yao ya msingi.

HOJA HIZI ZINATOSHA KUPINGA DABI KUPIGWA ZANZIBAR

 Hoja ya kwanza ni uwezo wa uwanja wa New amaan, ni uwanja mdogo ambao hauna uwezo wa kukidhi kubeba mashabiki Wengi ilihali uwanja wa Benjamini Mkapa unauwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 .

Hoja ya pili , gharama za usafiri kwa mashabiki kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar ni kubwa, hali inayoweza kupunguza idadi ya mashabiki watakaohudhuria kutoka Bara , shabiki kutoka mkoani atalazimika kusafiri mpaka Dar es laam Kisha achukue boti kuelekea Zanzibar jambo ambalo litakuwa gumu kwa Wengi .

Hoja ya tatu, Gharama za malazi na hoteli visiwani humo zimetajwa kuwa juu, jambo linaloongeza mzigo kwa wapenzi wa soka wanaotamani kushuhudia mchezo huo moja kwa moja, Hotel za Zanzibar zinahadhi ya juu hivyo hata gharama yake itakuwa kubwa ukilinganisha na maisha ya watanzania wa kawaida hawawezi kumudu.

Hivyo Kuna haja kwa bodi ya ligi kutathmini upya hatua hiyo kabla ya sintofahamu kutokea kwa sababu timu hizi mbili ndio kioo Cha ligi , na kama wakileta masihala kunaweza kushusha thamani ya ligi na mchezo wenyewe.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments