Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imethibitisha kuachana na mshambuliaji wake, Kibu Dennis, baada ya kufikia makubaliano ya uhamisho kwenda Al Nasr Benghazi ya nchini Libya.
Dili hilo limekamilika na Simba imeingiza kiasi cha dola za Marekani 300,000 sawa na takribani Shilingi milioni 772.8 za Kitanzania kutokana na mauzo ya nyota huyo.
Kibu , ameitumikia Simba kwa misimu minne na nusu, akitoa mchango mkubwa katika mashindano ya ndani na kimataifa , Uamuzi huo unaashiria mwisho wa safari yake ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Kariakoo.
Ilikuwa ni ndoto ya mchezaji huyo kutafuta malisho mapya kwa misimu kadhaa ikiwemo kufanya majaribio kwenye baaadhi ya timu lakini hakufanikiwa, hatimaye ndoto yake ya kucheza nje ya Tanzania imekamilika.
Katika klabu yake mpya, Kibu anatarajiwa kuungana na nyota wengine waliowahi kuitumikia Simba, akiwemo Fabrice Ngoma pamoja na Steven Mukwala ambao walisha cheza pamoja wakiwa Simba.
Tayali kibu Denis, ameshatambulishwa Al Nasry kuanza kuitumikia klabu hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment