Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Harry Kane ameendelea kuthibitisha ubora wake barani Ulaya baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata FC Bayern Munich wakiwa ugenini dhidi ya Werder Bremen .
Katika mchezo huo wa Bundesliga uliopigwa leo Februari 14, Kane alichangia matokeo Bora mchezo akitingisha nyavu mara mbili na kufikisha jumla ya mabao 500 katika soka la ushindani akiwa na vilabu na timu ya taifa.
Mshambuliaji huyo wa England sasa ana jumla ya mabao 280 aliyofunga akiwa na Tottenham Hotspur, 126 akiwa Bayern Munich, 78 akiwa na timu ya taifa ya England, huku mengine akiyafunga katika klabu za Millwall, Leyton Orient na Leicester City.
Ushindi huo umeifanya Bayern kuendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi huku Kane akiendelea kuwa tishio kwa safu za ulinzi za timu pinzani.
Kwa sasa, Kane anaonekana kuwa katika kiwango cha juu kabisa akithibitisha kuwa ni moja ya washambuliaji bora duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment