Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Jude Bellingham, atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja baada ya kupata jeraha la misuli kwenye mchezo wa Laliga dhidi ya Rayo Vallecano ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa 2-1.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Real Madrid, Bellingham amebainika kuumia misuli katika mguu wake wa kushoto, Jeraha hilo linamfanya nyota huyo wa England kukosa michezo muhimu ya timu hiyo.
Kutokuwepo kwa Bellingham ni pigo kwa Real Madrid, hasa ikizingatiwa mchango wake mkubwa msimu huu katika La Liga na mashindano ya Ulaya.
Timu ya madaktari inaendelea kufuatilia maendeleo yake huku akitarajiwa kurejea uwanjani baada ya kukamilisha programu ya matibabu na mazoezi maalum.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.jpeg)

Post a Comment