Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa na shirikisho barani Afrika imetamatika siku ya Jana Februari 15, 2026, kwa Kila timu kucheza michezo sita na tayali maji na mafuta yamekwisha jitenga kuelekea robo fainali huku timu nne wawakilishi wa Tanzania, jua likiwazamia hasubuhi kwenye mashindano hayo.
Tanzania iliingiza Jumla ya timu nne kwenye mashindano hayo, mbili zikiwa klabu bingwa na mbili Shirikisho, Simba na Yanga walikata tiketi kukipiga klabu bingwa ambapo mambo yamekuwa ndivyisivyo baada ya kujikuta wanatolewa mapema kwenye hatua ya makundi, hivyo hivyo kwa Azam na Singida kwa upande wa shirikisho .
Kwa Simba hii umeleta mshituko kwani kwa miaka ya hivi karibuni mnyama alizoeleka kufikia hatua ya robo fainali lakini kutokana na changamoto za hapa na pale wamejikuta wakiliona jua likizama hasubuhi kwenye michuano hiyo.
Kwa Yanga, hii inakua mara ya pili mfululizo kutoka hatua ya makundi wakiwa na alama nane zile zile , hii imeshangaza Wengi kwani kutokana na ubora wa kikosi Cha wananchi matarajio yalikuwa kuwaona wakivuka hatua hiyo angalau kufikia robo fainali, lakini mpira unadunda na bahati imetua kwa wapinzani.
Kwa upande wa Azam na Singida, wao wamejitahidi kutokana na wao ni wageni wa michuano hii hususani katika hatua ya makundi , kushindwa kwao hakutafsiri kuwa ni wabovu Bali ni fundisho na wamepata kuelewa michuano hiyo inachezwaje wakati mwingine watakuwa Bora zaidi.
ALAMA WALIZO MALIZA NAZO.
Yanga alama 8 nafasi ya tatu
Simba Sc alama 5 nafasi ya nne
Azam Fc alama 9 nafasi ya tatu
Singida alama 5 nafasi ya tatu.
Kwa mchanganuo huo wa alama klabu za Azam na Singida zinatakiwa kupewa pongezi kubwa kutokana na kuonyesha ukomavu licha ya ugeni wao kwenye mashindano wamevuna alama angalau zilizo onyesha kunakitu walikuwa wanahitaji ila bahati haikuwa kwao.
Kwa upande wa Simba na Yanga, hawajawatendea haki mashabiki wao kutoka kwao mapema ni uzembe mkubwa kwa sababu kwa sasa klabu hizi ni Moja klabu Bora na tishio barani Afrika , hivyo wanatakiwa kujitafakari msimu ujao wafanye vizuri.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.




Post a Comment