HIZI NI HISTORIA NGUMU KWENYE SOKA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika mchezo wa mpira wa miguu Kuna matukio mengi hutokea ambapo baadhi yake hugeuka na kuwa historia kutokana na ugumu wake au kutokea kwake kwa nadra, haya ni baadhi ya matukio yalitokea ambayo yalitengeza historia ngumu kwenye mchezo wa soka.

Sadio Mane -May 16, 2015

Historia yakipekee iliandikwa kwenye mchezo kati ya Southampton dhidi ya Aston Villa ambapo mshambuliaji wa Southampton kwa kipindi hicho Sadio Mane alifunga Hat trick ndani ya dakika 2 na sekunde 56 , ikiwa ni Hat trick ya haraka zaidi kuwahi kutokea ligi kuu nchini England.

Robert Lewandowski- Septemba 22, 2015.

Akiwa anaichezea Beyer munich dhidi ya Wolfsburg alitokea benchi na kuandika historia ya kipekee ambapo alifunga mabao matano ndani ya dakika tisa na kuwashangaza Wengi katika historia ya soka.

Lionel Messi - 2012

Ndani ya mwaka mmoja mchezaji huyo mwenye kipaji Cha ajabu akifanikiwa kufunga mabao 92 kwa ngazi ya klabu na timu ya Taifa, ambapo mabao 72 aliyafunga akiwa Barcelona na 13 alifunga akiwa na timu ya Taifa ya Argentina, huu ni wastani wa zaidi ya bao Moja kwa Kila mchezo alio cheza, na mchezaji kufikia mabao hayo inahitaji utimamu wa miwili na akili.

Historia zipo ili zivunjwe ila historia hizi ni baadhi ya historia ngumu zilizowekwa na magwiji hao wa soka ambao Bado wanacheza mpira mpaka sasa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments