Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha raia wa Argentina, Miguel Angel Gamondi, amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, akipewa jukumu la kuendeleza mafanikio yaliyoshuhudiwa katika kipindi kifupi alichokaimu nafasi hiyo , ambapo Hafla imefanyika February 16, 2026 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es laam.
Gamondi amepewa mkataba huo baada ya kuiongoza Stars kufuzu hatua ya 16 bora ya AFCON 2025 kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo, mafanikio yaliyoamsha matumaini mapya kwa soka la Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha timu ya taifa inafanya vizuri katika michuano ya kimataifa, hususan AFCON 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo huku akitoa wito kwa wachezaji wakitanzania waliopo nje ya nchi kuja kulipigania Taifa lao.
Aidha, Makonda alieleza kuwa malipo ya kocha huyo yatagharamiwa na Serikali kupitia ofisi ya Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya dhati ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo nchini.
Uteuzi huo unaongeza matumaini kwa mashabiki wa soka nchini, wakiamini uzoefu wa Gamondi utaleta mapinduzi chanya na kuiweka Tanzania katika ramani ya soka la Afrika na Duniani kwa ujumla.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment