FIFA YAIWEKEA TP MAZEMBE MARUFUKU YA KUSAJILI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeipiga marufuku klabu kongwe barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo, kusajili wachezaji wapya hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Adhabu hiyo haiashirii kufungiwa kabisa kwa shughuli zote za klabu, bali inalenga kusimamisha zoezi la usajili wa wachezaji wapya kwa kipindi ambacho hakijawekwa wazi, hadi pale klabu itakapokamilisha kikamilifu masuala yaliyoibuliwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa, marufuku hiyo ni sehemu ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na FIFA katika utekelezaji wa kanuni na udhibiti wa vilabu vilivyohusishwa na mizozano ya kisheria, kimkataba au kifedha ambayo haijatatuliwa kwa wakati.

FIFA, imeeleza kuwa zuio hilo litaendelea kuwepo hadi TP Mazembe itakapomaliza kikamilifu kushughulikia masuala yote yanayohusiana na kesi husika, kabla ya kurejeshewa haki ya kufanya usajili.

Hatua hiyo imeibua mjadala mpana katika duru za michezo barani Afrika, ikizingatiwa kuwa TP Mazembe ni moja ya vilabu vyenye historia kubwa na mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa, hususan Ligi ya Mabingwa Afrika.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments