DABI YA KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini yataelekezwa visiwani Zanzibar Machi 1, 2026, pale watani wa jadi Yanga na Simba SC watakapokutana katika dabi ya Kariakoo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26, ukiwa ni namba 54 , unatarajiwa kuanza saa 2:15 usiku na ni miongoni mwa michezo yenye mvuto mkubwa zaidi katika soka la Tanzania.

Kwa mara nyingine, dabi hiyo itachezwa nje ya Dar es Salaam, jambo linaloongeza hamasa kwa mashabiki wa Zanzibar na maeneo ya jirani kupata fursa ya kushuhudia moja kwa moja pambano hilo kubwa katika Uwanja wa New Amaan.

Wengi walizoea kuona pambano likipigwa Benjamin Mkapa lakini haitakuwa hivyo kutokana na wenyeji wa mchezo huo Yanga Sc kuamua kuupeleka mchezo huo Zanzibar.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments