COMO YA FABREGAS BALAA JIPYA SERIE A

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha wa Como Cesc Fabregas, ameendelea kuonyesha uwezo mkubwa wa ufundishaji baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Juventus katika mchezo wa Serie A uliopigwa leo.

Ushindi huo umeifanya Como kufikisha alama 46 wakiwa nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, hatua inayozidi kuwapa matumaini makubwa ya kufuzu michuano ya UEFA msimu ujao.

Chini ya Fabregas, Como imekuwa ikiontesha soka la kuvutia na lenye nidhamu ya hali ya juu, jambo ambalo limeanza kuwafanya wachambuzi wengi kuitaja timu hiyo kama moja ya vinara wa soka bora nchini Italia kwa sasa.

Mbali na mwenendo mzuri wa ligi, Como pia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Coppa Italia kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 40, ishara tosha ya mapinduzi makubwa ndani ya klabu hiyo.

Kwa mwendo huu, Como inaonekana kuwa tishio jipya Serie A huku ikiendelea kufukuzia nafasi za juu zitakazoipeleka kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments