Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Klabu ya Norway, Bodø/Glimt, imeendelea kushangaza bara la Ulaya baada ya kuonyesha makali katika michezo yao ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE wakiwalaza vigogo na kutinga hatua ya 16 Bora.
Licha ya kutocheza mechi za ligi tangu Novemba 30 , 2025 kutokana na mapumziko ya baridi Ligi Kuu ya Norway, Bodø/Glimt wamekuwa moto wa kuotea mbali katika michuano ya UEFA Champions League mwaka 2026.
Katika rekodi yao ya kuvutia:
Waliichapa Manchester City , mabao 3-1
Wakiwa ugenini wakaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Atletico Madrid
Kisha wakaiondosha Inter Milan kwa jumla ya mabao 5-2 (nyumbani na ugenini)
Matokeo hayo yamewapeleka rasmi katika Hatua ya 16 Bora, hatua ambayo hawakupewa nafasi ya kufikia na wamekuwa kama suprise package.
Kwa mwenendo wao wa sasa, Bodø/Glimt wanaonekana kuwa moja ya timu hatari zaidi katika michuano hiyo, wakithibitisha kuwa ukubwa wa jina sio kigezo cha mafanikio barani Ulaya.
Safari yao ya kusisimua inaendelea kuvuta hisia za mashabiki wengi, huku wengi wakisubiri kuona kama wataendelea kuandika historia zaidi katika hatua zinazofuata.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment