Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kalabu ya Arsenal yenye maskani yake jijini Londoni imeanza kuingia matatani kwenye mbio za kutwaa taji la EPL, siku ya Jana The Gunner walipata sare ya 2-2 dhidi ya Wolves wakiwa ugenini sare ambayo haikutarajiwa na Wengi kutokana na mizani ya timu zote mbili.
Sare hiyo inawafanya The gunners kudondosha alama mbili huku wapinzani wao wa karibu Man city wakihitaji kushinda mchezo unaofuata na kupunguza pengo la alama na kufikia alama mbili jambo ambalo linawapa Presha Arsenal kuelekea ubingwa.
Arsenal, wamekuwa na ugonjwa wa kuanza msimu vizuri lakini mwishoni waanza kupotea kwenye ramani ,na hali hii imeanza kuwatokea msimu huu.
The gunners wasipo ongeza umakini wanaweza kushushwa kileleni mwa msimamo kutokana na ratiba iliyopo mbele Yao.
MICHEZO INAYOFUATA YA ARSENAL
TOTTENHAM VS ARSENAL
ARSENAL VS CHELSEA
BRIGHTON VS ARSENAL
Michezo hii ni migumu na ndiyo itakayo toa hatima ya Arsenal kileleni huku matokeo ya City yakichagiza msukumo kwa wana London hao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment