Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports .
Klabu ya Young Africans imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kutawala soka la Tanzania na Afrika Mashariki baada ya kumsajili mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurelio Depu (25), raia wa Angola, akitokea klabu ya Radomiak Radom ya nchini Poland.
Depu ni mshambuliaji mwenye uzoefu mkubwa wa soka la ngazi ya juu, akiwa tayari amecheza katika ligi kadhaa kubwa na ngumu barani Ulaya, ikiwemo ligi ya Ureno, Serbia na Poland ligi zinazojulikana kwa ushindani, na ubora wa hali ya juu , Uzoefu huo unampa hadhi ya kuwa mchezaji aliyekomaa kiakili na kiufundi, tayari kukabiliana na presha ya klabu kubwa kama Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Depu amesaini mkataba wa miaka miwili, na anatarajiwa kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ya Wananchi, hasa kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Ujio wa Depu unaashiria wazi mkakati wa Yanga wa kusuka kikosi chenye mchanganyiko wa vipaji vya ndani na wachezaji wa kimataifa wenye uzoefu, ili kuendelea kushindana kwa nguvu kwenye Ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa.
Mashabiki wa Yanga sasa wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mshambuliaji huyo wa Angola atakavyotafsiri uzoefu wake wa Ulaya ndani ya jezi ya kijani na njano.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment